IQNA

Televisheni ya Algeria yakataa kuonyesha filamu ya Hassan na Hussein

16:03 - August 21, 2011
Habari ID: 2174750
Mkurugenzi wa kanali ya televisheni ya Qur'ani ya Algeria ametangaza kuwa kanali hiyo haitaonyesha filamu ya Hassan na Hussein AS na kusisitiza kuwa filamu hiyo haitaonyeshwa ili kuzia fitina nchini Algeria.
Muhammad Awadi amesema kuwa kanali ya televisheni ya Qur'ani ya Algeria inarusha hewani filamu mpya za kidini na imejiepusha kuonyesha filamu ya Hassan na Hussein ili kuzuia fitina kati ya Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni.
Filamu ya Hassan na Hussein iliyotengenezwa nchini Jordan imepingwa na maulamaa wengi wa Kiislamu wa madhehebu zote za Shia na Suni kutokana na kupotosha ukweli wa kihistoria na kujaribu kuwatetea maadui wa Watu wa Nyumba ya Myumba ya Mtume SAW. 847517
captcha