Akizungumzia hali ya Libya, Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa OIC ameeeleza kufurahishwa kwake na matukio ya hivi karibuni ya Libya na kuwapongeza wanamapinduzi kwa ushindi walioupata katika matukio hayo.
Huku akisema kuwa wananchi wa Libya wamejitolea na kupitia machungu mengi katika kufikai ushindi huo, Ihasanoglu amewatakia rehema ya Mwenyezi Mungu wale wote waliopoteza maisha yao kwenye matukio hayo na vilevile kuwatakia nafuu ya haraka majeruhi.
Vilevile amewataka Walibya wote kuchunga na kulinda umoja wa ardhi yao na kushirikiana na Baraza la Mpito kama mwakilishi pekee halali wa wananchi wa nchi hiyo. Amewataka pia wazingatie sheria za kitaifa na kimataifa na kutochukua hatua za kulipiza kisasi dhidi ya wenzao.
Ihsanoglu pia amewataka askari watiifu kwa Gaddafi kuweka chini silaha zao na kutii matakwa ya mabadiliko ya Walibya.
Mwishoni amezitaka nchi zote wanachama wa OIC kuwaunga mkono wanamapinduzi wa Libya. 848144