IQNA

Kuvunjiwa heshima Ayatullah Qassim ni kuvunjiwa heshima Mashia wa Bahrain

14:52 - August 27, 2011
Habari ID: 2177322
Kufuatia hatua ya Khalid bin Ali Aal Khalifa Waziri wa Sheria wa Bahrain ya kumwandikia barua ya dharau na vitisho Ayatullah Isa Qassim, kiongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Mashia wa Bahrain, wanazuoni na wanasiasa wa nchi hiyo wamelaani na kulalamikia rasmi hatua ya waziri huyo dhidi ya kiongozi huyo wa kidini.
Katika barua hiyo, waziri huyo wa sheria amemtuhumu Ayatullah Isa Qassim kwamba anavuruga na kutishia umoja wa kitaifa wa Bahrain kupitia hutuba zake za Swala ya Ijumaa.
Wanazuoni na wanasiasa wa Bahrain wamekemea vikali barua hiyo ya Khalid bin Ali na kuwataka watawala wa ukoo wa kifalme wa nchi hiyo kuheshimu wanazuoni na hasa Ayatullah Isa bin Qassim. Wamesema iwapo watawala hao wataendelea kumvunjia heshima Ayatullah Qassim au kumdhuru kwa njia yoyote ile Waislamu wa nchi hiyo watauteketeza ukoo huo wa kifalme.
Akitoa radiamali yake kuhusiana na barua hiyo ya dharau, Sheikh Mahmoud al-Aali, mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa Bahrain amesema kuwa barua hiyo inaonyesha wazi udhaifu mkubwa wa waziri huyo na utawala wa nchi hiyo katika kukabiliana na changamoto muhimu za kitaifa. Ameitaka serikali ya Manama badala ya kuwaandama wanazuoni wasio na hatia izingatie na kutatua matatizo halisi yanayohatarisha usalama wa kitaifa ikiwemo televisheni na magazeti yanayodhibitiwa na ukoo wa kifalme yanayochochea chuki nchini humo.
Sheikh al-Aali amesema vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na watawala wa Aal Khalifa vimekuwa vikichochea hitilafu za kimadhebeu ambapo vimekuwa vikiwataka wananchi wa nchi hiyo kupambana na Ushia pamoja na wafuasi wa madhehebu hiyo iliyo na wafuasi wengi zaidi nchini humo. Hii ni katika hali ambayo hakuna sehemu yoyote katika hotuba za Ayatullah Isa Qassim ambapo mwanazuoni huyo amewataka Wabahrain wapigane na kuchukiana kwa misingi ya kimadhehebu. 849936
captcha