IQNA

Togo yatangaza Jumatano kuwa siku ya Idul Fitr

11:36 - August 28, 2011
Habari ID: 2177913
Baraza la Waislamu la Togo limetoa taarifa likitangaza kuwa siku ya Idul Fitr nchini humo itakuwa Jumatano ya tarehe 31 Agosti.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, swala ya idi itaswaliwa rasmi siku hiyo katika miji yote ya nchi hiyo. Baraza hilo limewapongeza Waislamu wa nchi hiyo kwa mnasaba wa kuadhimishwa idi hiyo na kusema kuwa hiyo itakuwa fursa nzuri ya kuondoa chuki, kuimarisha mazungumzo ya maelewano kati ya wafuasi wa dini tofauti na kuimarishwa kwa utamaduni wa kuishi pamoja kwa amani wananchi wote wa Togo.
Asilimia 29 ya Watogo ni Wakristo, asilimia 20 Waislamu na asilimia 51 ni ya wafausi wa dini za kimila na kikabila. 850831
captcha