IQNA

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Lebanon:

Lengo la wasanii Waislamu ni kuwasilisha maana ya aya za Qur'ani katika fikra

15:32 - August 29, 2011
Habari ID: 2178848
Wakati msanii wa Kiislamu anapochora aya ya Qur'ani huwa na lengo la kuwasilisha maana ya aya hiyo katika fikra ya mtazamaji.
Hayo yamesemwa na Laila Hubar Saqr, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Lebanon katika mahojiano yake na IQNA mjini Tehran. Amesema kuwa madaa kuu ya kazi za kisanii za wasanii Waislamu ni aya za Qur'ani na lengo kuu huwa ni kuwasilisha maana ya aya hizo katika fikra za watu.
Bi Laila Hubar amesema kuwa sanaa ya Kiislamu haina mfungamano wowote na kabila, kaumu au kundi maalumu na kila mtu sawa awe Muislamu au la, anaweza kutengeneza kazi za kisanii zinazoakisi umaridadi wa Qur'ani.
Msanii huyo maarufu wa Lebanon amesema kuwa kila msanii mwenye mapenzi na Qur'ani Tukufu na kuwa na mfungamano na maneno ya Mwenyezi Mungu anaweza kuwafunza watu wengine mafundisho ya kitabu hiyo kupitia kalibu ya sanaa.
Vilevile ameashiria mchango muhimu wa sanaa ya Kiislamu katika kuimarisha umoja na mshikamano wa Kiislamu na akasema kuwa Qur'ani Tukufu ni kitabu kimoja chenye lengo moja la kumuongoza mwanadamu kuelekea kwa Mwenyezi Mungu na kwa msingi huo kinaweza kuwa nembo ya umoja na mshikamano wa Waislamu wote. 850585
captcha