IQNA

Walio na njaa Somalia waongezeka

22:07 - September 06, 2011
Habari ID: 2182629
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetangza kuwa njaa imetangazwa katika eneo la sita nchini Somalia huku takriban watu 750,000 wakikabiliwa na njaa kwa muda wa miezi minne ijayo.
Mashirika ya kutoa misaada yamekuwa yakisambaza misaada nchini Somalia kwa karibu watu milioni nne lakini huenda njaa ikasambaa kwa miezi inayokuja.
Taarifa ya Kituo cha Kuchunguza Usalama wa Chakula Somalia cha Umoja wa Mataifa imesema kuwa eneo la Bay ni eneo jipya la Somalia lenye tatizo la chakula, na kuongeza kwamba mamia ya Wasomali wanakufa kila siku kutokana na njaa nchini humo.
Wakati hayo yakiripotiwa magazeti ya Uturuki yametoa ripoti juu ya kuibiwa viungo vya watoto wa Kisomali na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Kwa mujibu wa magazeti hayo, utawala wa Kizayuni wa Israel unatumia fursa iliyopatikana ya mgogoro wa chakula nchini Somalia kuiba viungo vya watoto wa nchi hiyo wanaosumbuliwa na njaa. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hadi sasa viungo vingi ya watoto wa Somalia vimeporwa na kupelekwa Israel.
855910
captcha