IQNA

Waziri Mkuu wa Canada akosolewa kwa kuwashambulia Waislamu

18:41 - September 10, 2011
Habari ID: 2184567
Baraza Kuu la Kiislamu na Kongresi ya Kiislamu ya Canada zimetoa taarifa mbili tofauti zikikosoa matamshi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Stephen Harper kuhusu Waislamu.
Taasisi hizo mbili kubwa za Kiislamu nchini Canada zimemtaka Waziri Mkuu wa nchi hiyo kuwaomba radhi Waislamu baada ya kudai kuwa Uislamu ni hatari kwa Canada.
Taarifa la Baraza Kuu la Kiislamu la Canada imekosoa matamshi hayo ya Stephen Harper ikisema kuwa haikubaliki kabisa kwa kiongozi huyo kuufungamanisha Uislamu na makundi yenye misimamo ya kufurutu ada na imemtaka awaombe radhi Waislamu.
Sehemu moja ya taarifa hiyo imesema: "Matamshi ya Waziri Mkuu wa Canada yanawavunjia heshima Waislamu zaidi ya bilioni moja kote duniani."
Kogresi ya Kiislamu ya Canada pia imesema matamshi ya Harper yanawahujumu Waislamu na kwamba alipaswa kutumia maneno yanayofaa kubainisha hatari ya makundi yenye misimamo mikali. 857881

captcha