IQNA

Wito wa kufanyika maandamano makubwa ya kuuteka ubalozi wa Israel nchini Jordan

13:00 - September 12, 2011
Habari ID: 2185741
Wanaharakati wa Jordan wanaopinga kuboreshwa uhusiano wa nchi za Kiarabu na utawala haramu wa Israel wametoa wito wa kufanyika maandamano makubwa ya mamilioni ya watu kwa lengo la kuvamia na kuuteka ubalozi wa utawala huo mjini Amman, mji mkuu wa nchi hiyo.
Wito huo ambao umetolewa kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook unataka maandamano hayo yafanyike siku ya Alkhamisi tarehe 15 Septemba.
Watayarishaji wa maandamano hayo wanasema kuwa lengo lao la mwisho ni kufungwa ubalozi huo mjini Amman.
Kufuatia wito huo askari usalama wa Jordan wameimarisha usalama pambizoni mwa ubalozi huo ili kuzuia kukaririwa kitendo kama kile kilichotokea hivi karibuni mjini Cairo, Misri ambapo Wamisri wamevamia na kuharibu ubalozi wa utawala wa Kizayuni mjini humo. 859104
captcha