IQNA

Mafanikio ya Hizbullah yanatokana na kufuata mkondo wa Imam Khomeini

12:47 - September 13, 2011
Habari ID: 2186117
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema harakati hiyo imeweza kupata ushindi na kusimama kidete mbele ya Utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na kufuata mkondo wa harakati ya Imam Khomeini.
Naibu wa Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, wilaya na muqawama ni mihimili mikuu miwili ya kuendelea mwamko wa Kiislamu.
Sheikh Naim Qassim amesema hayo katika hotuba yake kwenye Mkutano wa Tano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt ulioanza Jumapili hapa mjini Tehran na kusisitiza kwamba, Waislamu wanapaswa kuandaa mazingira ya kudhihiri Imam Mahdi kwa ajili ya kuja kusimamisha uadilifu na usawa. Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah amebainisha kwamba, muqawama wa wananchi wa Lebanon ulisimama kidete na ndio maana ufanikiwa kupata ushindi dhidi ya Israel baada ya miongo 6.
Sheikh Naim Qassim amebainisha kwamba, Waislamu wa madhehebu ya Kishia wamekuwa wakiandamwa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel hivyo njia pekee ni kusimama kidete.
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ameashiria matukio ya nchini Bahrain na akaitaka serikali ya Manama kudiriki na kuitikia wito wa wananchi wa nchi hiyo wanaotaka mabadiliko.
captcha