Muungano wa vyama hivyo ambao unajumuisha vyama 17 vya kisiasa kikiwemo cha Ikhwanul Muslimeen, unataka sheria za uchaguzi zifanyiwe marekebisho na kuwazuia wafuasi wa Mubarak kushiriki kwenye uchaguzi huo.
Umesema unataka kubuniwa kwa sheria ambayo itazuia kikamilifu kurejea madarakani chama cha Mubarak pamoja na wafuasi wake na wakati huohuo kutoa fursa kwa vyama vya kisiasa ambavyo havijahusishwa na uhalifu na jinai dhidi ya taifa la Misri kushiriki kwenye uchaguzi uajo.
Sheria ya sasa ya Misri inatoa fursa kwa wafuasi wa Mubarak kushiriki kwenye uchaguzi kama wagombea huru. 861728