IQNA

Mubarak alikuwa na wasiwasi mkubwa wa kuenea Ushia katika Mashariki ya Kati

13:51 - September 22, 2011
Habari ID: 2191875
Shirika la Wikileaks limefichua kupitia nyaraka zake za siri kwamba Hosni Mubarak dikteta wa zamani wa Msiri aliyeng'olewa madarakani hivi karibuni nchini humo alikuwa na wasiwasi mkubwa wa kuenea Ushia katika Mashariki ya Kati.
Wakati huohuo shirika hilo limesema kuwa Mubarak alimwonya rais mwenzake wa Syria Bashar al-Assad kuhusiana na kudumishwa kwa shughuli za Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas pamoja na shughuli za kisiasa za mwakilishi wake Khalid Masha'al nchini humo. Alimtahadharisha kwamba kuendelea nchini humo kwa shughuli za Mash'al kungemgharimu sana kiongozi huyo wa serikali ya Damascus.
Dikteta huyo wa zamani wa Misri pia alisema kuwa aliingiwa na wasiwasi mkubwa wa kuenea na kupata nguvu Ushia katika Mashariki ya Kati na hasa katika nchi za Iraq, Bahrain, Saudia na Kuwait na kudai kwamba jambo hilo linahatarisha usalama wa eneo hili nyeti. 865398
captcha