IQNA

Rais Ahmadinejad akutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

11:50 - September 25, 2011
Habari ID: 2192527
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kuzungumza na Ban Ki-moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Wawili hao wamekutana pambizoni mwa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani na kujadili masuala muhimu ya kieneo na mabadiliko yanayojiri hivi sasa duniani. Ahmadinejad na Ban Ki-moon wamejadili pia nafasi ya Umoja wa Mataifa, changamoto na migogoro inayoikabili dunia hivi sasa na pia ulazima wa kufanyiwa marekebisho Umoja wa Mataifa.
Katika upande mwingine Rais Ahmadinejad wa Iran amesisitiza kuwa Baraza la Usalama halina uwezo wa kulinda haki za mataifa. Amesema kwamba Umoja wa Mataifa haujatekeleza majukumu yake ipasavyo suala linaloonesha kwamba umoja huo una udhaifu na matatizo ya kimuundo.
Rais wa Iran pia ameashiria kadhia ya wanadiplomasia wanne Wairani wanaoshikiliwa katika gereza za kuogofya za Utawala wa Kizayuni wa Israel. Amesema ushahidi unaonyesha wanadiplomasia hao waliotekwa nyara mwaka 1982 wako hai na hivyo amemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kufuatilia kadhia hiyo.
866553
captcha