IQNA

Wapalestina walaani hotuba ya Obama katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

11:51 - September 25, 2011
Habari ID: 2192535
Matabaka mbalimbali ya Palestina yamelaani vikali hotuba ya Rais Barack Obama wa Marekani aliyoitoa Jumatano iliyopita katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo aliuunga mkono wazi wazi utawala wa Kizayuni wa Israel.
Wanasiasa, wanaharakati na wananchi wa kawaida huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu wamelaani hotuba ya Obama na kubainisha kwamba, serikali ya Marekani haiwezi kuwa mpatanishi mwadilifu baina ya Wapalestina na Wazayuni.
Viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS wametangaza kuwa, wananchi wa Palestina hawana matumaini yoyote kwa serikali ya Marekani na wataendelea kupigania haki zao wao wenyewe.
Rais Barack Obama wa Marekani ambaye Jumatano iliyopita alifungua mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa alidai kuwa Wapalestina hawawezi kupata nchi huru kupitia Umoja wa Mataifa na kwamba njia pekee ya kufikia lengo hilo ni kufanya mazungumzo na Israel.
866202
captcha