IQNA

Wahubiri wa Kikristo waliochoma moto Qur’ani Tanzania wakamatwa

14:01 - September 26, 2011
Habari ID: 2193513
Polisi nchini Tanzania wamewakamata wahubiri wanne wa Kikristo, kwa tuhuma za kuiteketeza kwa moto Qur’ani Tukufu.
Hayo yalisemwa Septembe 22 na Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Liberatus Barlow , katika taarifa yake kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa.
Barlow alisema uchunguzi wa awali wa tukio hilo umethibitisha kuteketezwa kwa moto, Qur’ani Tukufu na makasisi hao wa Kanisa la Tanzania Assemblies.
Akifafanua kuhusu tukio hilo, Barlow alisema lilijitokeza baada ya wachungaji hao kwenda katika nyumba ya Husina Hamisi na kuchoma moto Qur’ani. Alisema katika mahojiano naye, Husina alikiri kuwa kitabu kilichochomwa moto na wachungaji hao ni Qur’ani Tukufu na kwamba kauli hiyo iliiungwa mkono na mtoto wa Husina mwenye umri wa miaka 10.
Kwa mujibu wa ofisa huyo wa polisi, wachungaji hao watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka.
866994
captcha