IQNA

Jeshi la utawala wa Kizayuni lakiri kushindwa kukabiliana na Hizbullah

12:01 - September 29, 2011
Habari ID: 2195397
Kamanda Mkuu wa jeshi la utawala haramu wa Israel amekiri katika kikao cha siri kushindwa jeshi hilo kukabiliana na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah.
Amesema hali hiyo imesababishwa na kutengewa bajeti ndogo bila kuzingatiwa nguvu kubwa ya kijeshi ya Hizbullah.
Akizungumzia suala hilo, Karmil Manasha mchambuzi wa masuala ya jeshi la Israel ameashiria taarifa iliyotolewa hivi karibuni na redio ya utawala huo na kusema kuwa ni wazi kuwa kama jeshi hilo halitaongezewa bajeti ya kijeshi itakuwa vigumu kwalo kukabiliana na nguvu ya kijeshi inayokuwa kila siku ya Hizbullah na kwamba hali hiyo inafanywa kuwa mbaya zaidi na mwamko wa Kiislamu unaoshuhudiwa katika nchi kadhaa za Kiarabu na hasa Misri, dhidi ya tawala za kidhalimu za nchi hizo ambazo kimsingi zinashirikiana na utawala wa Tel Aviv.
Manasha amesema kwamba makamanda wa ngazi za juu wa jeshi la Israel wana wasiwasi mkubwa kuhusiana na jambo hilo na kusisitiza kwamba kama hawataongezewa bajeti ya kijeshi bila shaka watashindwa kukabiliana na changamoto muhimu zinazowakabili katika eneo la Mashariki ya Kati na hasa Hizbullah. 869033
captcha