IQNA

Baraza Kuu la Kijeshi la Misri laitisha kikao cha dharura leo

17:04 - October 01, 2011
Habari ID: 2196700
Kufuatia maandamano makubya yaliyofanywa na Wamisri jana Ijumaa katika miji tofauti ya nchi hiyo chini ya anwani ya 'Ijumaa ya Kurejesha Mapinduzi' Baraza Kuu la Kijeshi la nchi hiyo limevitaka vyama vya kisiasa vya nchi hiyo kukutana nalo leo Jumamosi.
Baraza hilo limeitisha kikao hicho ili kujadiliana na vyama vya kisiasa masuala mbalimbali yayohusiana na uchaguzi na kipengee cha tano cha sheria ya uchaguzi. Vyama karibu vyote vya Misri vinapinga sheria ya uchaguzi na wala havikubaliani na marekebisho madogo yaliyofanyiwa sheria hiyo inayoruhusu waungaji mkono wakuu wa dikteta wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak kugombea viti vya bunge katika uchaguzi ujao.
Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa uamuzi wa Baraza la Kijeshi wa kuitisha kikao hicho ni dalili tosha inayothibitisha kuwa maandamano yaliyofanywaq na wananchi jana yalikuwa na athari kubwa ya kisiasa.
Vyama kadhaa vimetishia kususia uchaguzi ujao iwapo kipengee cha tano cha sheria ya uchaguzi hakitabadilishwa.
Watu 15 walijeruhiwa katika maandamano hayo yaliyofanyika karibu na makao makuu ya baraza hilo. Waandamanaji walifanya maandamano kutangaza upinzani wao dhidi ya kutekelezwa tena sheria ya hali ya hatari, kuhukumiwa raia katika mahakama za kijeshi na kutaka marekebisho ya sheria ya uchaguzi pamoja na kurejeshwa madaraka mikononi mwa raia.
Wamisri pia walifanya maandamano makubwa katika makao makuu ya baraza hilo katika mji wa Alexandria na kumtaka Tantawi mkuu wa baraza hiyo ang'atuke madarakani. 870477
captcha