IQNA

Matukio ya Mashariki ya Kati yameudhoofisha utawala ghasibu wa Israel

13:54 - October 05, 2011
Habari ID: 2199534
Matukio yanayojiri kwa sasa katika eneo la Mashariki ya Kati hususan hatua ya kufukuzwa mabalozi wa Israel katika nchi za Misri na Uturuki yameuweka utawala ghasibu wa Israel katika hali mbaya sana na kuudhoofisha zaidi.
Hayo yamesemwa na David Morrison ambaye ni mwanachama wa Muungano wa Ireland na Palestina (The Ireland Palestine Alliance). Ameliambia shirika la IQNA kwamba Israel inaikalia kinyume cha sheria ardhi ya Palestina kwa zaidi ya miaka 60 na wakati huo huo inazungumzia suala la kufanya mazungumzo na Wapalestina. Morrison amesema tatizo kuu la Palestina ni uvamizi wa kijeshi wa Israel na mazungumzo yoyote yatakayofanyika hayawezi kuwa na natija maadamu tatizo hilo lingalipo.
David Morrison ameashiria matukio ya hivi karibuni katika eneo la Mashariki ya Kati na kusema kuwa matukio hayo hususan kufukuzwa mabalozi wa Israel huko Uturuki na Misri yameuweka utawala huo ghasibu katika hali mbaya mno.
Amesema ulimwengu umo katika mabadiliko na matukio ya sasa yanaonyesha kwamba nguvu za kidhahiri za Marekani zinayoyoma na kutoweka.
Mwanaharakati huyo wa kisiasa na mtetezi wa haki za Wapalestina amekosoa pia uungaji mkono na himaya ya nchi za Magharibi kwa utawala ghasibu wa Israel na akasema kuwa nchi za Magharibi hususan Maekani zinafumbia macho jinai na uhalifu unaofanywa na Israel na zimekuwa zikizuia kupasishwa hata azimio moja dhidi ya utawala huo ghasibu.
Amehoji kwamba ni kwa nini nchi za Magharibi zinaituhumu Iran kuwa inafanya jitihada za kumiliki silaha za nyuklia ilhali hazina ushahidi wowote wa madai hayo na wakati huo huo zinafumbia macho silaha za nyuklia za utawala haramu wa Israel? 873403

captcha