IQNA

Marekani yadai:

Njia ya haraka zaidi ya kuhamisha madaraka ya nchi huko Yemen ni kujiuzulu Saleh

15:14 - October 05, 2011
Habari ID: 2199596
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ameendeleza siasa za kindumakuwili za serikali ya Washington kwa ajili ya kupora na kuteka nyara mapinduzi ya wananchi wa Yemen kwa kudai kuwa njia ya haraka ya kufikia awamu ya kuhamisha madaraka ya nchi hiyo ni kujiuzulu Rais Abdullah Saleh.
Victoria Noland amewaambia waandishi habari kwamba hatua muhimu zaidi yakuchukuliwa katika kipindi cha kuhamisha madaraka ya nchi huko Yemen ni kuamiliana na Makamu wa Rais wa nchi hiyo Abdurabuh Mansur Hadi.
Noland amesema Washington inaamini kwamba njia ya haraka ya kuiondoa Yemen katika mgogoro wa sasa ni Abdullah Saleh kutia saini mpango wa amani uliobuniwa na nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi.
Nchi za Magharibi zinaendelea kuingiliaji kati katika harakati za mapinduzi ya wananchi wa Mashariki ya Kati na siku chache zilizopita Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ambaye nchi yake ilifanya juhudi kubwa za kutaka kuteka nyara mapinduzi ya wananchi wa Misri na kujaribu kupotosha mwelekeo wake, alidai kuwa Washingtn itashirikiana na serikali mpya ya Misri hata kama itakuwa ya Kiislamu! 874060

captcha