IQNA

Mkuu wa Baraza la Kijeshi la Misri asema kuna uwezekano mdogo wa kufutwa sheria ya hali ya hatari

15:59 - October 08, 2011
Habari ID: 2199876
Mkuu wa Baraza la Kijeshi la Misri amesema kuwa kuna uwezekano mdogo wa kufutwa sheria ya hali ya hatari nchini humo katika hali ya hivi sasa.
Gazeti linalochapishwa nchini Lebanon la Intiqad limemnukuu Muhammad Hussein Tantawi akibainisha suala hilo na kusisitiza kwamba kufutwa sheria hiyo ni jambo lisilowezekana katika mazingira yanayotawala nchini humo hivi sasa na kwamba jambo hilo litawezekana tu pale hali hiyo itakapobadilika.
Tantawi amezungumzia suala hilo katika hali ambayo bunge la Misri limerefusha muda wa utekelezwaji wa sheria hiyo kwa kipindi kingine cha miaka miwili huku wananchi na vyama vya kisiasa vya nchi hiyo vikilalamika na kufanya maandamano makubwa ya kulishinikiza baraza hilo la kijeshi lifutilie mbali sheria hiyo ya kiukandamizi. 874031
captcha