IQNA

Baada ya kuvunjiwa heshima Mashia:

Mwandishi wa Saudia ataka kuuzuliwa khatibu wa Masjidunnabi SAW

15:00 - October 09, 2011
Habari ID: 2201635
Mwandishi wa gazeti la al Watan la Saudi Arabia Abdur Rahman al Wabili amepinga matamshi yaliyowavunjia heshima na kuwadhalilisha Waislamu wa madhehebu ya Shia yaliyotolewa na khatibu wa Msikiti Mtukufu wa Mtume SAW mjini Madina na ametoa wito wa kuuzuliwa shekhe huyo wa Kiwahabi na kuvuliwa uongozi wa Swala za jamaa katika msikiti huo mtakatifu.
Al Wabili amesema kuwa matamshi yaliyotolewa na Sheikh Ali al Hudhaifi yanawavunjia heshima Waislamu wote wa madhehebu ya Shia duniani na matamshi hayo yanahesabiwa kuwa ni jinai dhidi ya binadamu kwa mujibu wa sheria za Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu.
Mwandishi huyo amesisitiza kuwa mtu yeyote anayechochea na kuhamasisha jinai dhidi ya binadamu anapaswa kufikishwa mahakamani.
Al Wabili amesema kuwa watu wanaoongoza swala za jamaa katika misikiti miwili mitukufu (ya Makka na Madina) wanapaswa kuwaheshimu wafuasi wa madhehebu zote za Kiislamu la sivyo wauzuliwe kutoka katika maeneo hayo matukufu.
Mwandishi huo wa Kisaudi amesema, hotuba zinazovunjia heshima matukufu ya Mashia zinazotolewa na Ali al Hudhaifi katika Msikiti wa Mtume SAW mjini Madina ni mfano wa njama za kutaka kuzusha fitina za kimadhehebu kati ya raia wa Saudi Arabia.
Katika hotuba zake za Swala ya Ijumaa iliyopita kwenye Msikiti wa Mtume SAW mjini Madina, Sheikh Ali al Hudhaifi alitoa matamshi ya kudhalilisha akisema kuwa Mashia ni makafiri na wameondoka katika dini ya Mwenyezi Mungu.
Matamshi hao yamewakasirisha mno maulamaa, waandishi na wasanii wa Saudi Arabia. Sheikh Hassan Saffar ambaye ni kiongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Saudia na Imam wa Ijumaa wa msikiti wa mji wa Qatif amelaani vikali matamshi hayo na kusema kuwa maulamaa wa Kiwahabi wanataka kuzusha fitina za kimadhehebu nchini humo. 876145

captcha