IQNA

Wayemen wakaribia kupata ushindi baada ya dikteta wa nchi hiyo kwenda nje ya nchi

15:45 - October 10, 2011
Habari ID: 2202481
Mwanaharakati mmoja wa masuala ya sheria wa Yemen amesema mapinduzi ya wananchi wa nchi hiyo yanakaribia kupata ushindi baada ya Rais Abdullah Saleh wa nchi hiyo kwenda nje ya nchi.
Ghazi al Saami' amesema kuwa siku ya kihistoria inayosubiriwa na Wayemen kwa miaka mingi, inakaribia.
Al Saami' ameyasema hayo baada ya Rais Abdullah Saleh wa Yemen kuondoka nchini huko na kwenda Ujerumani kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kwa ajili ya matibabu.
Mwanasheria huyo wa Yemen amesisitiza kuwa mapinduzi ya wananchi yatadumisha mwenendo wa amani na kwamba kama Wayemen wangetaka kuuondoa madarakani utawala wa kiimla wa Saleh basi ungekuwa tayari umeng'olewa madarakani.
Amesisitiza kuwa wananchi wanamapinduzi wa Yemen wametimiza asilimia 75 hadi 80 ya matakwa yao na kwamba utawala wa kidikteta wa Abdullah Saleh unakaribia kusambaratika. Amesema familia ya dikteta huyo inataka kuitumbukiza Yemen katika vita na machafuko. 877191


captcha