Kufuatia machafuko yaliyoshuhudiwa hivi karibuni nchini Misri, Ahmad Tayyib, Sheikh wa al-Azhar amewataka viongozi wa Kiislamu na Kikristo wa nchi hiyo kufanya mazungumzo ya maelewano.
Amesema viongozi wa pande mbili hizo wanapasa kufanya mazungumzo ya haraka ili kumaliza mgogoro uliopo na kuepusha ghasia zinazoweza kutokea baadaye nchini humo. Amesema uchunguzi kuhusiana na chanzo cha machafuko ya hivi karibuni kati ya Wakristo na Waislamu ndiyo njia pekee itakayosuluhisha mivutano inayotokea mara kwa mara kati ya pande hizo.
Akizungumzia ghasia hizo Isam Sharaf, Waziri Mkuu wa Misri alisema jana Jumapili kwamba tishio kubwa zaidi linalotishia usalama wa Misri ni kugonganishwa Wakristo na Waislamu na pia wananchi na jeshi la nchi hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti, watu 24 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa jana baada ya Wakristo wa Kikopti wa Misri waliokuwa na hasira kubwa kufuatia tukio la kuchomwa moto kanisa lao katika eneo la as-Swaid, kukabiliana na polisi ya kuzua fujo. 877086