Ripoti hiyo ambayo pia imechapishwa na gazeti la Guardian la Uingereza inasema kuwa Mfalme Hamad bin Isa Aal Khalifa wa Bahrain amekuwa na uhusiano mkubwa na wa muda mrefu na shirika hilo la ujasusi la Wazayuni.
Gazeti hilo pia limenukuu nyaraka za Wikileaks zinazosema kuwa Muhammad Hussein Tantawi, Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Misri ambaye hivi sasa ni mkuu wa Baraza la Kijeshi la nchi hiyo amekuwa kizuizi kikubwa katika juhudi za Israel za kusimamisha magendo ya silaha kuelekea Ukanda wa Gaza.
Nyaraka hizo pia zinaashiria wasiwasi wa mmoja wa makamanda wa ngazi za juu katika jeshi la Israel aliyesema hivi karibuni kwamba Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah, ina uwezo mkubwa wa kijeshi wa kuweza kuishambulia Israel kwa makombora 20,000. 877244