IQNA

Katibu Mkuu wa ISESCO aonana na Waziri wa Utamaduni na Utalii wa Azarbaijan

14:51 - October 12, 2011
Habari ID: 2203756
Abdul Aziz Othman at-Tuweijri, katibu Mkuu wa Shirika la Elimu Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ISESCO, jana Jumanne alionana na kuzungumza na Abdul Fadhl Qarayev, Waziri wa Utamaduni na Utalii wa Jamhuri ya Azarbaijan.
At-Tuweijri ameoana na kuzungumza na waziri huyo akiwa nchini humo kuhudhuria kikao cha kimataifa kinachofanyika chini ya anwani ya 'Karne ya 21, Matarajio na Matatizo.'
Pande mbili hizo zilijadiliana na kuchunguza mipango ya kuandaliwa kikao cha saba cha Mawaziri wa Masuala ya Utamaduni wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC.
Vilevile wamesisitiza umuhimu wa kuandaliwa mipango madhubuti kwa ajili ya kukifanikisha kikao hicho ambacho kinatazamiwa kufanyika huko Algeria.
Viongozi wawili hao pia wamejadili masuala mengine muhimu yanayohusu ulimwengu wa Kiislamu na vikwazo vinavyowakabili Waislamu katika pembe mbalimbali za duania.
At-Tuweijri pia alionana na kuzungumza na Waziri wa Elimu wa Azarbaijan na kusisitiza umuhimu wa kuimarishwa ushirikiano wa pande mbili kwa madhumuni ya kunyanyua viwango vya elimu katika nchi za Kiislamu. 878340
captcha