Kwa mujibu wa tovuti ya Arabic.China, maktaba hizo zimezinduliwa kwenye misikiti hiyo kwa lengo la kutoa fursa kwa Waislamu wa eneo hilo wanufaike na maendeleo ya kielimu na pia kuwawezesha wafanye utafiti wa kielimu na kiutamaduni kahusiana na masuala tofauti.
Zaidi ya vitabu 50,000 vinavyozungumzia masuala mbalimbali ya kisanaa, kijamii, kiutamaduni, kisheria na kidini vimewekwa kwenye maktaba hizo.
Televisheni na mitambo ya kucheza DVD pia imewekwa kwenye misikiti hiyo na mamlaka ya eneo hilo la Ninghai.
Akifafanua suala hilo Imam Mashao Chung wa Msikiti wa Liming katika jimbo hilo la Ninghai amesema kuwa maktaba hizo zitakuwa na nafasi muhimu katika kurahisisha juhudi za Waislamu wa eneo hilo kupata maarifa tofauti ya Kiislamu na kunyanyua viwango vyao vya kiutamaduni.
Inasemekana kuwa zaidi ya Waislamu milioni mbili wa eneo hilo ni kutoka kabila la Hui ambalo linaunda zaidi ya thuluthi moja ya Waislamu wote wa eneo hilo. 878612