Yusuf Ahmad amesema kuwa Syria haitashiriki katika taarifa yoyote itakayotolewa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ikiilaumu Iran kutokana na madai hayo yasiyokuwa na msingi ya Marekani.
Amesema Saudia Arabia ni nchi ndugu na jirani na Syria lakini taarifa yoyote itakayotolewa na jumuiya hiyo dhidi ya Iran kwa kutegemea madai ya uongo ya Marekani inapaswa kutegemea ushahidi wa kweli na si urongo mtupu.
Mwishoni mwakilishi wa Syria katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amezitahadharisha nchi hizo na njama za Marekani za kutaka kuzitumia kama fimbo dhidi ya Iran na kwa ajili ya kufikia malengo yake makhsusi. 880236