Talal Utreisi, mtafiti na mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Lebanon, amesema kuwa matamshi ya Ayatullahil Udhma Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na tuhuma za hivi karibuni za Marekani dhidi ya serikali ya Tehran yanabainisha wazi kwamba Iran iko tayari kukabiliana na njama pamoja na tuhuma hizo.
Akizungumza na televiesheni ya al-Manar ya Lebanon, Utreisi ambaye pia ni mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kistratejia ya nchi hiyo amesema maneno ya Kiongozi Muadhamu yanabainisha wazi kwamba Iran imevunjilia mbali, kwa dalili madhubuti, tuhuma hizo zisizo na msingi na kwamba imeiweka Marekani katika hali ngumu ya kuthibitisha madai hayo dhidi yake.
Amesema Iran ni nchi pekee katika ulimwengu wa Kiislamu ambayo inatumia maneno kama hayo ya ujasiri dhidi ya mataifa makubwa ya Magharibi bila kuhofu jambo lolote.
Mhadhiri huyo amesisitiza kwamba msimamo wa Iran mbele ya tuhuma za hivi karibuni za Marekani na washirika wake wa Kiarabu imethibitisha wazi kwamba Tehran haiwezi kulazimishwa kusalimu amri mbele ya njama na tuhuma zisizo na msingi za Wamarekani. 880589