IQNA

Uadilifu wa kijamii, takwa la waandamanaji katika miji 950 ya dunia

16:32 - October 17, 2011
Habari ID: 2206649
Waandamanaji wamefanya maandamano katika miji 950 katika nchi 82 za dunia na kutaka kutekelezwa uadilifu wa kijamii na kupambana na mfumo wa ubepari duniani.
Kwa mujibu wa televisheni ya Aljazeera, maandamano hayo yamefanyika katika nchi hizo zilizo katika mabara ya Marekani, Ulaya, Asia na Afrika. Ili kuratibu na kufungamanisha maandamano hayo, waandaaji wa maandamano hayo wameanzisha tovuti kwa jina la 'tumeungana kwa ajili ya kuleta mabadiliko duniani' ambapo wamesisitiza kwamba wataendelea kufanya maandamano kwa madhumuni ya kupigania haki na demokrasia yao.
Waandamanaji hao wamesema wataendeleza maandamano hayo ili kupinga sera mbovu za viongozi wao wa kisiasa na mabepari ili kujiainishia wenyewe mustakbali wao.
Waandamanaji wanasisitiza kwamba hawatakubali tena kutumiwa na wanasiasa kama vyombo vya kufikia malengo yao ya kisiasa na kwamba wanasiasa hao na mabepari wanaowaunga mkono wanapasa kutambua kwamba wakati wa mataifa kuungana na kujiamulia hatima yao yenyewe umefika. 881075
captcha