Amesema kuwa harakati za mapinduzi zinazoendelea katika nchi kadhaa za Kiarabu zitakuwa na athari kubwa katika mustakbali wa Mashariki ya Kati.
Akizungumza jana Jumapili na televisheni ya al-Alam, Bi Basma amesema kuwa ubadhirifu huo wa Saudia ni sehemu ya ufisadi mkubwa zaidi ulioenea katika nchi za Kiarabu na kuongeza kuwa Saudia inapasa kujiepusha kuingilia masuala ya ndani ya Bahrain na Yemen kwa sababu hali inayotawala sasa katika eneo hairuhusu uingiliaji huo wa kisiasa na kijeshi.
Huku akikiri kwamba uingiliaji wa Saudia nchini Bahrain haukupasa kufanyika, amedai kwamba Saudia imeingilia masuala ya ndani ya Yemen kutokana na kuwepo jamii kubwa ya Wayemen nchini humo na vilevile matatizo yaliyoko mwenye mpaka mrefu wa pamoja wa nchi hizo. Amesema jumuiya za nchi za Kiislamu na Kiarabu hazijatoa suluhisho lolote la maana kuhusiana na mgogoro wa Yemen ili kuchukua nafasi ya Saudi Arabia nchini humo.
Ameyataka mataifa ya Kiislamu kuungana na kushirikiana ili kukabiliana na njama za nchi za Magharibi dhidi ya umma wa Kiislamu. Amesema nchi hizo za Magharibi zimekuwa zikitekeleza mipango maalumu ya kunufaika na utaalamu na vipawa vya Waislamu badala ya wataalamu hao wa Kiislamu kuandaliwa mazingira ya kuyanufaisha nchi zao wenyewe.
Bintimfalme Basma bint Saud amewataka wananchi wa nchi za Kiarabu kubuni mipango ya kujiendeshea maisha yao wenyewe na kujichagulia viongozi wawatakao bila ya kutishwa na mtu yeyote. 881315