Aun al-Khasawneh ambaye ameteuliwa na Mfalme Abdallah II kuunda serikali mpya ya nchi hiyo baada ya kumfuta kazi Maaruf al-Bakhit, amesema kuwa atayashirikisha makundi yote ya kisiasa ya Jordan, likiwemo kundi la Ikhwanul Muslimeen katika serikali yake mpya ili kuandaa uwanja wa kuwepo ushirikiano mzuri kati ya Wajordan wote katika ujenzi wa nchi.
Amesema, Ikhwanul Muslimeen ni sehemu ya jamii na historia ya Jordan na daima wamekuwa wakitaka kuimarisha usalama na uthabiti wa nchi hiyo.
Waziri Mkuu mpya huyo amesema kuwa kipaumbele cha serikali yake kitakuwa ni kupambana na ubadhirifu na ulaji-rushwa serikalini tatizo ambalo amesema limekuwa likiitatiza nchi hiyo kwa muda mrefu.
Al-Khasawneh kabla ya uteuzi wake huo amekuwa akihudumia Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC iliyo na makao makuu yake mjini The Hague, Uholanzi. 882043