Kwa mujibu wa tovuti ya Islamophobia, tamasha hilo limepangwa kufanyika kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Waislamu ya Uswisi na Kituo cha Utamaduni cha misikiti na taasisi za kidini za nchi hiyo.
Lengo la kufanyika kongamano hilo la kitaifa ni kuwabainishia Waislamu na wasio Waislamu wa nchi hiyo maana ya ubaguzi na chuki dhidi ya Uislamu, ufafanuzi wa mifano ya ubaguzi wa kimbari unaofanywa dhidi ya Waislamu nchini Uswisi na nchi nyingine za Ulaya, kuwasihi Waislamu waripoti vitendo vya ubaguzi vinavyofanywa dhidi yao kwa vyombo husika vya kisheria na pia kuuarifisha Uislamu kwa wasiokuwa Waislamu.
Waandaaji wa tamasha hilo wanataraji kuwa viongozi wa kisiasa na kiutamaduni wa Uswisi walioalikwa kushiriki kwenye tamasha hilo watachukua hatua za kutosha ili kukabiliana na vitendo vya chuki na ubaguzi dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo.
Wanataraji pia kwamba wataweza kuvishawishi vyombo vya habari vya nchi hiyo ambavyo kwa kawaida huchochea hisia za kibaguzi na chuki dhidi ya Waislamu virekebishe tabia zao na kuwashawishi wananchi wa nchi hiyo kuishi pamoja kwa amani bila kujadili mbari wala dini zao.
Mbali na wanafikra na wanazuoni wa Kiislamu, viongozi wa kisiasa na kiutamaduni wa serikali ya Uswisi wamealikwa pia kuzungumza katika tamasha hilo. 882023