IQNA

Wabunge wa Malaysia waonya dhidi ya kuenea makundi ya wahubiri wa Kikristo

14:22 - October 19, 2011
Habari ID: 2208064
Mbunge mmoja wa Malaysia ameonya dhidi ya kuenea kwa makundi ya uhubiri wa Kikristo nchini humo, makundi ambayo yameimarisha juhudi zao katika siku za hivi karibuni kwa malengo ya kuwafanya Waislamu kuwa Wakristo.
Mbunge Ibrahim Ali ameitaka Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo pamoja na taasisi za kidini kuchukua hatua za dharura kwa ajili ya kusimamisha mwenendo huo.
Akifafanua suala hilo, Ibrahim Ali, mbunge huru wa bunge la Malaysia amesema kuwa wizara hiyo pamoja na mashirika ya kidini ya Malaysia yanapasa kutekeleza majukumu yao vilivyo na kuchukua hatua za kuwalinda Waislamu wasiokuwa na ufahamu mkubwa wa mafundisho ya dini yao ambao ndio wanaolengwa zaidi na makundi hayo ya uhubiri wa Kikristo.
Vilevile ameitaka serikali kuchukua hatua za lazima kusaidia kuimarisha mafundisho na itikadi za Kiislamu nchini na hivyo kujaribu kuzuia hatari ya uhubiri wa Kikristo ambao anasema unahatarisha usalama wa jamii ya nchi hiyo ambayo kimsingi ni ya Kiislamu. Amesema hivi karibuni viongozi wa Kikristo katika makanisa machache ya nchi hiyo wamekuwa wakiwashawishi wafuasi wao kuimarisha juhudi za kuwafanya Waislamu kuwa Wakristo hadi pale nchi hiyo itakapobadilika na kuwa ya Kikristo.
Mbunge Ibrahim Ali amesema polisi ya nchi hiyo imemkabidhi nyaraka zinazothibitisha kwamba viongozi wa Kikristo wa vyama vya kisiasa vya nchi hiyo wamekuwa wakihudhuria makanisani na kuahidi kwamba watafanya juhudi kubwa za kuhakikisha kwamba waziri mkuu ajaye wa nchi hiyo atakuwa Mkristo. 882470
captcha