Kongamano hilo limetayarishwa na Sekritarieti ya Jumuiya ya Kimataifa ya Uislamu kwa ushirikiano wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Indonesia.
Kongamano hilo litafunguliwa kwa hutoba ya Rais Susilo Bambang Yudhoyono wa nchi hiyo.
Abdallah bin Abdul Muhsin at-Turiki Katibu Mkuu wa jumuiya iliyotajwa amesema kwamba kongamano hilo litafanyika katika hali ambayo ulimwengu wa Kiislamu unashuhudia vitisho na migogoro mingi. Amesema katika kipindi hiki cha teknolojia na maenedeleo ya Kielimu, vyombo vya habari vya nchi za Kiislamu vinapasa kushirikiana zaidi ili kufikia malengo yao.
Amesema lengo kuu la kufanyika kongamalo hilo ni kuufikishia ulimwengu ujumbe muhimu wa mafundisho ya Kiislamu na kuufahamisha kwamba mafundisho hayo yana athari kubwa katika kutatua matatizo na changamoto muhimu za dunia. 883056