Mkuu wa baraza hilo ametoa sifa hizo alipokutana hivi karibuni na ujumbe wa wabunge wa Hizbullah katika bunge la Lebanon huko Moscow. Mufti huyo amesema kwamba Hizbullah imepata mafanikio hayo makubwa kutokana na uongozi shupavu wa Sayyid Hassan Nasrullah.
Katika safari hiyo wabunge hao wa Lebanon pia wamekutana na kuzungumza na viongozi wa ngazi za juu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ambapo wamejadili na kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali ya Lebanon, Mashariki ya Kati na ya kimataifa.
Katika mazungumzo hayo viongozi wa Russia wamesisitiza tena uungaji mkono wao kwa juhudi zinazofanywa na viongozi wa Lebanon kwa madhumuni ya kulinda kujitawala taifa hilo na kuyasihi makundi yote ya kisiasa ya nchi hiyo kuongeza jitihada zao za kuimarisha mazungumzo ya makundi ya kidini na kisiasa kwa shabaha ya kuboresha demokrasia nchini.
Vilevile wameyaonya madola makuu dhidi ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi za Mashariki ya Kati. 883945