Tarehe 25 Januari mwaka huu wa 2011 ilikuwa siku ya kwanza ya mapinduzi ya wananchi wa Misri dhidi ya utawala wa kidikteta wa Hosni Mubarak na kudumishwa mwamko wa Kiislamu uliokuwa umeanzia Tunisia.
Baraza la Serikali ya Misri chini ya uongozi wa Isama Sharaf Waziri Mkuu wa muda wa nchi hiyo limechukua uamuzi wa kuienzi siku hiyo kwa kuitangaza kuwa ni siku ya mapumziko ya kitaifa.
Siku hiyo taasisi na jumuiya zote za serikiali zitafungwa.
Tarehe 25 Januari mwaka huu wananchi wa Misri walianza harakati za maandamano na malaamiko dhidi ya serikali ya kidikteta ya kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak. Watu wasiopungua 850 waliuawa katika maandamano na malalamiko ya siku 18 na hatimaye maandamano hayo yalimlazimisha dikteta Mubarak kuondoka madarakani.
884572