IQNA

Madaktari wa Kishia wahukumiwa kwenye mahakama za rufaa

15:32 - October 24, 2011
Habari ID: 2211004
Madaktari, wauguzi na wafanyakazi 20 wa hospitali za Manama huko Bahrain ambao wamekuwa wakituhumiwa kuunga mkono harakati za mapinduzi za Mashai wa nchi hiyo walihukumiwa jana Jumapili katika mahakama ya rufaa ya mji huo.
Televisheni ya al-Manar imeripoti kwamba licha ya kuwa maafisa wa vyombo vya mahakama vya Bahrain awali walikuwa wametangaza kuwa kesi ya watuhumiwa ingesikilizwa kwenye mahakama za kiraia lakini bado kesi yao imesikilizwa kwenye mahakama ya kijeshi.
Licha ya ahadi iliyotolewa na viongozi wa vyombo vya sheria vya Bahrain ya kufuatiliwa kesi ya madaktari na wafanyakazi waliotajwa kwenye mahakama za kiraia, lakini wamefikishwa kwenye mahakama za kijeshi na kuhukumiwa vifungo vya muda mrefu wa kati ya miaka 5 hadi 15 jela.
Vifungo hivyo dhidi ya watuhumiwa hao waliokuwa wakifanya kazi katika Hospitali ya Salmania ambayo ni hospitali kubwa zaidi katika mji wa Manama, vimeyakasirisha mno mashirika ya kutetea haki za binadamu, Umoja wa Mataifa na nchi kadhaa za Magharibi. 885906
captcha