IQNA

‘Kuporomoka tawala za kidikteta’, maudhui kuu ya katuni za maonyesho ya kimataifa ya magazeti Tehran

22:21 - October 25, 2011
Habari ID: 2211834
Kuporomoka kwa madikteta wa Kiarabu kama Hosni Mubarak wa Misri, Muammar Gaddafi wa Libya, Zainul Abidin bin Ali wa Tunisia na Saddam Hussein wa Iraq ndiyo maudhui kuu ya katuni na vibonzo vya Maonyesho ya Kimataifa ya Magazeti yaliyoanza leo hapa mjini Tehran.
Sehemu ya vibonzo na katuni ya maonyesho hayo imesheheni picha za katuni zenye maudhui kama kung’olewa madarakani Hosni Mubarak, kukimbia nchi rais wa zamani wa Tunisia Zainul Abidin bin Ali, ushindi wa wanaharakati wa Kiislamu nchini Tunisia, kutoroka kwa Gaddafi na kukutwa katika mfereji wa maji machafu na kufananishwa picha hiyo na ile ya kunaswa dikteta wa zamani wa Iraq Saddam Hussein akiwa amejificha shimoni na kadhalika.
Sehemu hiyo pia ina picha ya rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak akiwa katika jeneza huku Anwar Sadat rais wa zamani wa Misri aliyetia saini mkataba wa amani wa Camp David na utawala ghasibu wa Israel akimkaribisha. 887171

captcha