IQNA

Dola laki moja zatengwa kwa ajili ya mtu atakayeteka askari wa Israel

16:24 - October 26, 2011
Habari ID: 2212451
Sheikh Audh al Qarani mufti mwenye misimamo ya wastani wa Saudi Arabia ametenga zawadi ya dola laki moja kwa mtu yeyote atakayeteka nyara askari wa utawala ghasibu wa Israel.
Sheikh al Qarani ambaye ni miongoni mwa wanazuoni mashuhuri na wenye misimamo ya wastani wa Saudia amesema katika ukurasa wake wa Facebook kwamba atatoa zawadi ya dola laki moja kwa mtu atakayemteka nyara askari wa utawala ghasibu wa Israel na kwamba lengo la hatua hiyo ni kubadilishana askari hao na Wapalestina wanaoshikiliwa katika korokoro za kutisha za Israel.
Sheikh Audh al Qarani ametoa wito huo kujibu hatua iliyochukuliwa na Walowezi wa Kizayuni ya kutenga zawadi nono kwa mtu yeyote atakayewaua kigaidi mateka wa Kipalestina walioachiwa huru siku chache zilizopita kutoka kwenye jela za Israel.
Wito huo wa Sheikh al Qarani umekaribishwa sana na wanaharakati wengi katika mtandao wa Facebook na tayari watu wasiopungua mia saba wamempongeza mwanazuoni huyo kwa kutenga zawadi hiyo. 887799

captcha