Ismail Hania amempigia simu Katibu Mkuu wa chama hicho Rashid al Ghanushi na kumpongeza kwa ushindi huo ambao amesema utahudumia pia malengo ya taifa la Palestina.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na serikali ya Hamas, Rashid al Ghanush amewatunuku wananchi wa Palestina ushindi wa chama chake cha al Nahdha nchini Tunisia na kusema kuwa mapambano ya kishujaa ya watu wa Ghaza katika mashambulizi ya Israel yamewaathiri mno Waislamu kote duniani.
Waziri Mkuu wa Palestina amesema kuwa baada ya kuanza mwamko wa Kiislamu Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika kumetukia mambo mawili yaliyowafurahisha Waislamu kote duniani ambayo ni kukombolewa mateka wa Kipalestina na ushindi wa chama cha Kiislamu cha al Nahdha nchini Tunisia. 887913