Kwa mujibu wa gazeti la Sharqul Ausat, jambo hilo limetangazwa na Turki bin Sultan ambaye ni naibu mkuu anayesimamia masuala ya utamaduni na upashaji habari nchini Saudia. Ameashiria kutumika teknolojia mpya katika suala la upashaji habari huko Saudia na kuongeza kuwa viongozi wa nchi hiyo watafanya juhudi kubwa katika kuwahudumia vizuri mahujaji.
Abdul Aziz Abdul Khaliq az-Zahrani, afisa anayesimamia masuala ya vyombo vya habari katika uwanja wa ndege wa Abdul Aziz amesema kwamba Wizara ya Utamaduni na Vyombo vya Habari ya Saudia imetuma wafanyakazi 130 kwa ajili ya kuwahudumia mahujaji katika uwanja huo. Ameongeza kuwa tayari magazeti kadhaa ya nchi hiyo yamechapishwa kwa lugha tofauti za dunia ili kuwapasha habari mahujaji kuhusiana na mambo tofauti yenye manufaa kwao katika kipindi cha hija.
Afisa huyo amesema kuwa vyombo 18 tofauti vya upashaji habari kwa njia ya picha vimewekwa katika uwanja uliotajwa wa ndege ili kuwapasha habari za hija kwa lugha tofauti mahujaji wanaokwenda Makka kuhiji. 891178