IQNA

Mahakama ya kijeshi ya Misri yatoa hukumu dhidi ya wahusika wa shambulio la ubalozi wa Israel

17:17 - November 02, 2011
Habari ID: 2216525
Mahakama ya kijeshi ya Misri imetoa kifungo cha kusalia nyumbani cha miezi sita kwa watu waliohusika na shambulio la ubalozi wa utawala haramu wa Israel mjini Cairo.
Kwa mujibu wa televisheni ya al-Manar, mahakama hiyo ilitoa hukumu hiyo dhidi ya watu 73 waliopatikana na hatia ya kutekeleza shambulio hilo hapo mwezi Septemba uliopita na kuwaachilia wengine wawili kwa kutopatikana na hatia.
Mahakama iliyotajwa ya Misri imetoa hukumu hiyo dhidi ya watuhumiwa hao ambao inasema ndio waliohusika moja kwa moja na shambulio hilo lililopelekea watu watatu kupoteza maisha na wengine 1049 kujeruhiwa.
Wamisri waliushambulia ubalozi huo katika kulalamikia hatua ya utawala haramu wa Israel ya kuua polisi 6 wa nchi hiyo. Kufuatia shambulio hilo, wanadiplomasia na wafanyakazi wa Kizayuni waliokuwa katika ubalozi huo walilazimika kukimbia na kuihama Cairo ili kuokoa maisha yao.
Hata hivyo walirejea mjini humo baada ya siku 10 na kuanza kutekeleza shughuli zao kama kawaida. 891820
captcha