IQNA

Ubelgiji mwenyeji wa kikao cha kieneo cha 'Septemba 11; Uislamu na Ulaya'

18:57 - November 05, 2011
Habari ID: 2217922
Kikao cha kieneo cha 'Septemba 11; Uislamu na Ulaya' kimepangwa kufanyika mjini Brussels nchini Ubelgiji tarehe 25 Novemba.
Kwa mujibu wa tovuti ya Euro-Muslims.eu, kikao hicho kimetayarishwa na Jamii ya Waislamu wa Ulaya EMN kwa uenyekiti wa Tariq Ramadhan, mtaalamu wa masuala ya Kiislamu mkazi wa Uswisi na kitafanyika katika Chuo Kikuu cha Saint Louis.
Wahadhiri na wataalamu wa masuala tofauti kutoka nchi za Norway, Ubelgiji, Italia, Hispania, Uholanzi, Uingereza, Ufaransa na nchi nyinginezo za Ulaya wamealikwa kushiriki katika kikao hicho.
Washiriki wa kikao hicho watajadili na kubadilishana mawazo kuhusiana na athari za matukio ya Septemba 11 kwa jamii ya Waislamu barani Ulaya na mtazamo wa watu wasiokuwa Waislamu kuhusiana na matukio hayo na vilevile Waislamu.
Matukio hayo na suala la kuenea chuki dhidi ya Waislamu barani Ulaya na nafasi ya makundi yenye misimamo ya kupindukia ya mirengo ya kulia ya kuzidisha chuki hiyo pia ni mambo yatakayopewa kupaumbele katika mijadala ya kikao hicho. 892916
captcha