IQNA

Mkuu wa Chuo cha Imam Sadiq nchini Iraq atekwa nyara

10:13 - November 06, 2011
Habari ID: 2218231
Vyombo vya usalama vya Iraq vimeripoti kuwa mkuu wa Chuo Kikuu cha Imam Sadiq (as) nchini humo ametekwa nyara katika mkoa wa Karkuk.
Habari zinasema kuwa watu waliokuwa na silaha na mavazi ya kijeshi wamemteka nyara mkuu wa Chuo Kikuu cha Imam Sadiq (as) Mussa Mustafa pamoja na mhadhiri wa chuo hicho Sami Ridha.
Mussa Mustafa alitekwa nyara na watu hao wasiojulikana akiwa nyumbani kwake.
Vyombo vya usalama vya Iraq vinalituhumu kundi la Ansar al Sunna kundi ndilo lililowateka nyara wahadhiri hao wa chuo kikuu na kwamba siku kadhaa zilizopita kundi hilo lilitawanya makaratasi yanayochea fitina za kimadhehebu likiwataka watu kuwashambulia Mashia wa Kiturkman na Wakurdi. 893851


captcha