Najib Razak ambaye yuko Saudi Arabia kutekeleza ibada ya Hija amesisitiza suala hilo katika ujumbe wake wa salamu za Idulhaji na kuongeza kuwa, japokuwa Waislamu wana utamaduni na kaumu tofauti na wanaishi katika nchi mbalimbali lakini wote ni sehemu ya mwili mmoja.
Waziri Mkuu wa Malaysia amesema kuwa ibada ya Hija inayowashirikisha Waislamu kutoka maeneo yote ya dunia ni nembo ya umoja na mshikamano wa Kiislamu na kwamba Mtume Muhammad (saw) pia alisisitiza juu ya umoja huo katika hotuba zake kwenye hija yake ya mwisho.
Amesema kuwa Waislamu kote duniani wanaweza kupata mafanikio makubwa iwapo watalinda umoja na mshikamano wao. 893817