IQNA

Wito wa kuundwa jumuiya ya uchumi wa Kiislamu

16:11 - November 08, 2011
Habari ID: 2219262
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wawekezaji wa Kiarabu Jamal Bayyum ametoa wito wa kuundwa Jumuiya ya Uchumi wa Kiislamu kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Fiqhi ya Kiislamu na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC).
Gazeti la Madina linalochapishwa nchini Saudi Arabia limemnukuu al Bayyumi akisema kuwa jumuiya ya uchumi wa Kiislamu inaweza kujumuisha pamoja wataalamu wa uchumi wa Kiislamu kutoka maeneo yote ya dunia na kuundwa kupitia uchaguzi huru.
Ameongeza kuwa jumuiya hiyo itawajibika kutilia maanani suala la ustawi wa kiuchumi katika nchi za Kiislamu, kuondoa vizingiti vya maendeleo ya kiuchumi na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi katika ya nchi za Kiislamu.
Amesema kuwa umma wa Kiislamu katika kipindi cha sasa ni sawa na mgonjwa anayehitajia tiba ili aweze kupambana na mipango ya nchi za Magharibi katika medani ya uchumi. 894869
captcha