IQNA

Ammar al Hakim:

Kondoka Marekani nchini Iranq ni chachu ya ujenzi mpya wa nchi hii

16:11 - November 08, 2011
Habari ID: 2219263
Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq Sayyid Ammar al Hakim amesema kuwa kuondoka majeshi ya Marekani nchini humo ni chachu inayowahamasisha Wairaqi kuijenga umpya nchi yao na kulinda usalama na amani.
Ammar al Hakim ambaye alikuwa akihutubia waumini katika swala ya Idi jana katika mji mtakatifu wa Najaf alisema kuwa matukio yanayojiri katika nchi za Kiarabu ni mwanzo wa awamu mpya katika maisha ya mataifa ya nchi hizo na yametikisa mataji ya watawala madhalimu.
Amesisitiza kuwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu inapaswa kuwa na muundo mpya unaolingana na mahitaji ya kipindi cha sasa.
Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq amesema kuwa Iraq ya baada ya kuondoka majeshi ya Marekani inaweza kujilinda yenyewe na kuondoka huko kwa Marekani ni chachu ya kuijenga upya nchi na kuimarisha zaidi amani na usalama.
Vilevile amesisitiza juu ya udharura wa kusafishwa vyombo vya usalama kutokana na watu waovu na kuimarishwa taasisi za upelelezi nchini Iraq. 894816
captcha