Khalid Said ambaye ni miongoni mwa watayarishaji wa maandamano hayo amesema kuwa maandamano hayo yamefanyika kupinga msimamo rasmi wa serikali ya Ufaransa ambayo inakutambua kuvunjiwa heshima Mtume wa Uislamu kuwa ni uhuru wa kusema na kujieleza.
Khalid Said ameongeza kuwa Waislamu wa Misri wataanza kususia bidhaa za Ufaransa kutokana na msimamo wa serikali ya Paris wa kuunga mkono picha hizo zinazovunjia heshima matukufu ya Kiislamu.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa gazeti la kila wiki la Charlie Hebdo na lile la Liberation yanayochapishwa nchini Ufaransa wiki iliyopita yalichapisha picha zinazomdhalilisha na kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza. Kitendo hicho kimewakasirisha mno Waislamu wa Ufaransa na maeneo mbalimbali duniani. 897152