Holder amesema mafundisho yanayotolewa kwa polisi yakieleza kuwa Uislamu ni dini ya kutumia mabavu na ya kikatili si sehemu ya mipango ya masomo ya polisi ya Marekani na kwamba yatakuwa na taathira mbaya na kukwamisha jitihada za kuimarisha maelewano na kuamilia vyema na Waislamu wa nchi hiyo.
Waziri wa Sheria wa Marekani ambaye alikuwa akihutubia Baraza la Seneti la nchi hiyo amesisitiza kuwa, Waislamu wa Marekani ni washirika muhimu katika mapambano dhidi ya ugaidi. Ameongeza kuwa inasikitisha kuona mafundisho kama hayo ya kupiga vita Uislamu yakitolewa katika jeshi la polisi la Marekani.
Septemba mwaka huu gazeti la Wired la Marekani lilifichua kwamba jeshi la polisi la nchi hiyo linapewa mafunzo ya kuupiga vita Uislamu. 896433