IQNA

Palestina yaitaka UNESCO kulinda maeneo matukufu ya Waislamu

11:35 - November 13, 2011
Habari ID: 2221627
Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imelitaka Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kutekeleza wajibu wake wa kulinda maeneo matukufu na turathi za Waislamu wa Palestina mbele ya mashambulizi yanayoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel.
Mustafa al Sawwaf anayesimamia Wizara ya Utamaduni ya Palestina amesema UNESCO inawajika kwa sasa kutekeleza wajibu wake kuhusu haki za Wapalestina kuliko wakati wowote mwingine hususan baada ya Palestina kutambuliwa rasmi kama mwanachama kamili wa shirika hilo la kimataifa.
Amesema kuwa mashambulizi yaliyofanywa hivi karibuni na jeshi la utawala ghasibu wa Israel dhidi ya makaburi ya kihistoria ya Maamanullah katika mji unaokaliwa kwa mabavu wa Quds ni sehemu ya mipango ya utawala huo ghasibu ambayo inapaswa kukomeshwa.
Taasisi ya Wakfu na Turathi ya al Aqsa pia imelaani hujuma hiyo ya utawala haramu dhidi ya makaburi ya kihistoria ya Maamanullah na imezitaka nchi za Kiislamu kulinda maeneo matukufu ya Waislamu mbele ya mashambulizi ya Wazayuni. 897515


captcha