Mahakama ya Misri imewapiga marufuku wanachama wa chama cha NDP kushiriki katika uchaguzi ujao kufuatia uamuzi wa hapo awali wa kuvunjwa chama hicho na kutaifishwa mali na milki zake.
Hussein Hamuda ambaye ni mtaalamu wa masuala ya kisiasa ya Misri amekaribisha hatua hiyo ya mahakama ya Misri na akatahadharisha kwamba maafisa wa serikali ya zamani ya nchi hiyo wanafanya njama za kuvuruga uchaguzi wa bunge.
Hussein Hamuda amesema kuwa baadhi ya viongozi wa utawala uliong'olewa madarakani nchini Misri na vyama vyenye uhusiano na maafisa hao wanafanya njama za kuharibu mwenendo wa uchaguzi nchini kwa kutumia udhaifu uliopo hivi sasa katika upande wa masuala ya usalama.
Uchaguzi wa bunge la Misri utafanyika mwishoni mamwezi huu wa Novemba. 897447